Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aahidi ushindi mbele ya Geita Gold

Gamondi Press Gamondi aahidi ushindi mbele ya Geita Gold

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina ameahidi kuibuka na ushindi katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kuanzia saa 10 jioni.

Gamondi amesema katika mchezo wa kesho, yeye na vijana wake watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo kuwapa furaha mashabiki wa Yanga licha ya kutopata muda mwingi wa kujiandaa.

“Maandalizi kwa upande wetu siyo mazuri sana kutokana na ratiba lakini sisi ni wataalamu na ligi kuna muda inakuwa na ratiba ngumu, lazima kuwa tayari.

“Leo tutakuwa na mazoezi jioni, ambayo yatatusaidia kuona hali ya wachezaji kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold.

“Nafahamu kesho tutakuwa na mchezo mgumu na sijui hali ya uwanja ikoje, lakini nafikiri itakuwa kama uwanja wa mchezo wetu uliopita.

“Ukweli nina wasiwasi sana na viwanja pamoja na maamuzi ya waamuzi uwanjani, nina imani kutakuwa na mabadiliko kwenye hili kwa sababu kila kitu kinaonekana wazi.

“Tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu, lakini mashabiki wameendelea kuwa pamoja nasi na kutupa sapoti kama vile bado hatujapoteza mchezo wowote, ni kazi yetu sasa kuhakikisha kwenye mchezo wa kesho tunajitoa kwa nguvu zote kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: