Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Yanga ya makombe na burudani inakuja

Fh Gamondi Gamondi: Yanga ya makombe na burudani inakuja

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutarajia mabadiliko zaidi ya uchezaji kwa timu yake tofauti na walivyoishuhudia kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs katika Tamasha la Kilele cha Siku ya Mwananchi Jumamosi.

Akizungumza na mwandishi wetu, Gamondi alisema anahitaji marekebisho madogo kwenye timu yake na anaamini timu hiyo itaendeleza makali yake kwenye ligi na mashindano ya kimataifa.

"Mashabiki wa Yanga wataendelea kufurahi, naamini kikosi hiki kitafanya vizuri kwenye mashindano yote, yapo marekebisho kidogo nitayafanya mazoezini na timu itakapoonekana kwa mara nyingine mashabiki wataona mabadiliko, nina wachezaji wenye uwezo mkubwa sana," alisema Gamondi.

Alisema siku zilizobaki kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu kuanza hapo Agosti 15, mwaka huu, atazitumia vizuri kuweka kile anachokitaka ndani ya timu hiyo na kuwataka mashabiki kujiandaa kupata furaha.

Alipoulizwa ni mapungufu gani aliyoyaona ndani ya timu hiyo, Gamondi hakutaka kuweka wazi lakini alisisitiza lazima wachezaji wake watengeneze nafasi nyingi za kufunga na wazitumie ipasavyo.

"Siwezi kusema, lakini kama kocha nina ramani yangu kichwani ya namna timu ninavyotaka icheze... ni lazima tutumie vizuri kila nafasi tunayoitengeneza, kwa sasa bado timu haijakaa vizuri kwa namna ninavyotaka," alisema Gamondi.

Aidha, alisema ameguswa na uwezo wa wachezaji wake na ana uhakika wataumpa matokeo mazuri kwenye mashindano watakayoshiriki.

Kikosi hicho cha Yanga kuinaendelea na maandalizi yake kwenye kambi waliyoiweka Avic Town Kigamboni kujiandaa na michezo ya Ngao ya Jamii na Ligi Kuu kwa ujumla wake.

Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Yanga itafungua pazia dhidi ya Azam FC Agosti 9, huku Simba wakicheza na Singida Fountain Gate FC Agosti 13 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: