Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Yanga ni hatari kwenye kushambulia, nataka tufuzu CAFCL bila kuruhusu bao

Gamondi Chama Aziz Pacome Gamondi: Yanga ni hatari kwenye kushambulia, nataka tufuzu CAFCL bila kuruhusu bao

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa miongoni mwa malengo yake ni kufuzu hatua inayofuata ya CAFCL bila kufungwa bao hata moja. Gamondi amesema hayo kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Vital'O ya Burundi utakaopigwa kwatika Dimba la Azam Complex.

Gamondi amesema ana kikosi kipana chenye wachezaji wengi bora lakini hilo halimfanyi akawadharau Vital'O licha ya kuwafunga bao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali CAFCL.

“Siwezi kuzungumzia timu nyingine lakini Yanga imekuwa timu bora kwenye kila idara, tazama msimu uliopita tulifunga mabao mengi sana lakini ndiyo timu iliyoruhusu mabao machache ya kufungwa kwenye ligi, hata CAFCL tuliruhusu mabao machache sana. Yanga ni hatari kwenye kushambulia lakini ni wazuri kwenye kuzuia kufungwa.

“Kila mechi ina mpango wake, tumedhamilia kufuzu hatua inayofuata bila kuruhu bao lakini ninaheshimu uwezo wa timu nyingine ambao ni wapinzani wetu. Kwenye soka lazima uwe professional na Yanga tupo kwenye level ya juu ya professional kwa hiyo siwezi kusema kwamba hatuwezi kufungwa bao tano lakini uhalisia hatuwezi kufungwa bao tano.

“Kwenye soka huwezi kujua, kila kocha ana maoni yake lazima umheshimu mwenzako. Kwangu na kwetu tutakuja kucheza mchezo seriously na kutafuta matokeo. Tuna mamilioni ya mashabiki kwa hiyo hatutaki kuwanyong’onyesha Wananchi.

“Kesho ninaamini itakuwa mechi ya kushambuliana kwa wote (open game) kwa sababu wenzetu hawana cha kupoteza. Mchezo uliopita walikuwa wanalinda sana lango lao japo tulifanikiwa kumiliki mpira na kuwafungua tukapata mabao, ninaamini kesho watashambulia zaidi kwa sababu wanataka mabao na hiyo itakuwa faida kwetu,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live