Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Yanga na Mamelodi ni vilabu bora Afrika

Gamondi X Mokwena Gamondi: Yanga na Mamelodi ni vilabu bora Afrika

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema bado wana nafasi ya kusonga mbele hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwakuwa wana mchezo wa marudiano katika Uwanja wa Loftus Versfeld Aprili 05, 2024 ndani ya Jiji la Pretoria nchini Afrika Kusini.

Akizungumza mara baada ya kutamatika dakika 90' za Robo Fainali ya CAFCL kati ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns, Gamondi amesema matokeo ya mchezo huu ni mipango yake kuwaruhusu Mamelodi kucheza zaidi katika eneo lao, ambacho hakina madhara kimatokeo.

"Tulipaswa kushinda mchezo. Tumecheza vizuri, tumetengeneza nafasi ila hatukuweza kuzitumia," amesema Mokwena.

Akizungumzia kuhusu mchezo ulivyokuwa, Gamondi amesema ulikuwa mchezo mgumu kati ya timu bora barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live