Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Wengi walitubeza kuwa hatutatoboa kwenda robo

Aziz Diarra Okrah Gamondi Yanga K Gamondi: Wengi walitubeza kuwa hatutatoboa kwenda robo

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa watu wengi waliibeza timu yake kuwa kutokana na ugumu wa kundi alilokuwepo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hawataweza kutoboa kwenda robo fainali lakini jambo hilo wameweza.

Gamondi amesema hayo jana Jumamosi, Februari 24, 2024 baada ya kutamatika kwa mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad na kuwafunga bao 4-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

"Tunashukuru Mungu kwa hatua hii kwanza na hongera kwa Wananchi. Binafsi Nimefurahi sana kuona Yanga inafuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25.

"Watu wengi walitubeza kuwa hatuwezi kufuzu kutokana na ugumu wa kundi letu, ila sisi kama timu tuliamini kwa umoja wetu, nguvu zetu kwa pamoja Kutoka kwa viongozi wetu, wanachama na mashabiki wote wa Yanga kwa pamoja tutafuzu.

"Mashindano haya ya Ligi ya Mabingwa siyo mepesi hata kidogo ila kwa level, ukubwa wa Yanga ni lazima tulijiandaa kufuzu ili tutumize malengo yetu. Wapinzani wetu leo hawakuwa wabaya ila ubora wa wachezaji wangu ndio umeamua mchezo.

"Watanzania wanapaswa kuelekea mpira wa Afrika kwa Sasa umekuwa sana naweza kusema hivyo. Ni wazi sasa hata Yanga nao wamefanya vizuri kwenye sekta ya uwekezaji ili kuweza kuipa nguvu timu kushindana na vilabu vingine vikubwa ambavyo vimewekeza vyema kwenye mashindano haya," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live