Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Walidhani kuondoka kwa Mayele Yanga itateseka

Mayele Gamondiii Gamondi: Walidhani kuondoka kwa Mayele Yanga itateseka

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo cha kikosi Yanga kutomtegemea mtu mmoja katika kufunga magoli, kimeonekana kumfurahisha zaidi Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye amefichua kwamba, anafurahishwa na jambo hilo.

Katika kikosi cha Yanga, kila mchezaji ana uwezo wa kuamua matokeo wakati wa mechi kwa kufunga magoli na wala si kuwategemea washambuliaji pekee.

Ukiangalia mechi mbili za Ligi Kuu ya NBC msimu huu ambazo wamefunga magoli 10, wafungaji ni tofauti wakiwemo mabeki Yao Attohoula na Dickson Job, viungo Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki na Maxi Nzengeli, huku pia washambulia Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni wakifunga.

Gamondi amesema: “Kwangu mimi kitu cha muhimu ni timu kushirikiana, ninapenda kumiliki mpira, napenda kucheza soka la kushambulia na kutoa burudani kwa mashabiki.

“Kama utaona matokeo na watu wanazungumza mengi kwamba tunafunga mabao mengi, katika mechi mbili za kwanza ukiangalia unaona wachezaji wengi wanaweza kufunga.

“Wachezaji wanafunga na safu ya ulinzi inazuia vizuri, hii ndiyo aina ya soka ninalopenda kuona tukicheza, tuna muda mwingine wa kuendelea kuwa bora zaidi.

“Ukiwa kama kocha, wachezaji wasipofuata falsafa zako inakuwa ngumu kufanikiwa, wachezaji waliopo Yanga wanafanya vizuri, nashukuru kwa hilo, wanafuata falsafa zangu na ninaamini watu wanafurahia.

“Inafahamika kazi ya straika ni kuuweka mpira katika nyavu, lakini kila mchezaji ana kazi hiyo akiwa uwanjani ingawa kazi kubwa ya straika ni kufunga.

“Najua kila mtu anadhani hivi sasa Yanga hayupo Mayele (Fiston), hivyo tutateseka sana, lakini nina wachezaji ambao kila mmoja anaweza kufunga, Clement Mzize anafunga, Musonda anafunga, Konkoni anafunga, Maxi, Aziz, kila mmoja anaweza kufunga.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: