Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Wachezaji wangu walikuwa wamechoka

Gamondi Sureboy Gamondi: Wachezaji wangu walikuwa wamechoka

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa wamepoteza mchezo kutokana na makosa ambayo wameyafanya katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kupoteza kwa kufungwa bao 2-1.

Gamondi pia amesema kuwa ilikuwa lazima kufanya Rotation ya kikosi kutokana na uchovu wa wachezaji wake wengi hivyo ilikuwa haina jinsi.

"Tumepoteza mchezo kutokana na makosa yetu. Golikipa (Diarra) alifanya makosa pia. Uwanja ulikuwa na changamoto.

"Baada ya goli la pili kilichofuata sio mpira. Simlaumu mwamuzi lakini wenzetu walikuwa ni kama hawataki kucheza tena mpira, mara wakae, wajiangushe, lakini nadhani tumepoteza kwa makosa yetu wenyewe.

"Nilifanya rotation' (Wachezi 7 kikosini) kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa ilikuwa lazima kufanya hivyo kutokana na uchovu wa wachezaji wangu wengi hivyo ilikuwa haina jinsi.

"Tutarejea tukiwa imara zaidi. Tumepoteza mchezo lakini hatujapoteza mashindano," amesema Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: