Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tutampiga Al Ahly kwao, tunataka tuongoze kundi

Gamondi Yanga Pacome Aziz Maxi Skudu Gamondi na wachezaji wake.

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa baada ya kufanikiwa kuwafunga CR Belouizdad kwa bao 4-0 hapo jana na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa akili yake imehamia kwa Al Ahly ambaye watacheza naye mchezo wa mwisho.

Gamondi amesema hayo jana Jumamosi, Februari 24, 2024 baada ya kutamatika kwa mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad na kuwafunga bao 4-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao utapigwa weekendijayo.

"Tunakwenda Misri (kuwafuata Al Ahly) bila kujali kama tumefuzu tayari ila tunakwenda kupambana kutafuta matokeo chanya ambayo yatatupa uongozi wa kuongoza kundi letu.

"Nimekaa Afrika zaidi ya miaka 15 sasa, wow kwa Tanzania watu wanapenda sana timu zao mpira unakuwa siku hadi siku kwangu mimi kama kocha ni furaha kufanya kazi na Yanga, klabu ambayo inaniunga mkono kwa nyanja zote. Asanteni sana Wanayanga," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live