Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tunazitaka alama tatu za Tabora United

Gamondi Bacca 6972d12 Ganindi na Bacca

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa kikosi cha Yanga SC, Miguel Angel Gamondi, amesema haitakuwa rahisi kupambana na Tabora United, lakini malengo yao ni kuondoka na pointi tatu.

Gamondi ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho Jumamosi ambapo Yanga itakuwa ugenini kumenyana na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mchezo huo unakuja ikiwa timu ya Yanga juzi Jumatano imetoka kuifunga Medeama ya Ghana magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Tumejiandaa kadiri ya uwezo wetu kwa sababu unajua kucheza kila baada ya siku tatu inakuwa si rahisi kujiandaa vizuri kwa mechi, lakini tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunahitaji kupata pointi tatu.

“Unapocheza mechi za kimataifa kisha ukaja kucheza ligi, jambo gumu linakuwa kwa wachezaji miili yao kurejea kwenye hali ya kawaida, kufahamu mchezaji gani yupo katika hali nzuri na kuwafuatilia wapinzani.

“Tunajaribu kufanya tuwezavyo ili kuwa tayari kwa mechi. Hili ni soka na unapoifundisha timu kama Yanga unapaswa kuwa tayari kwa hilo.

“Wachezaji nao ni binadamu, wanachoka, wanapata majeraha na adhabu, wakati mwingine unapaswa kubadilisha mchezaji, hivyo lazima timu iwe na mabadiliko.

“Lomalisa (Mutambala) bado ni majeruhi, hayupo tayari kucheza, amechukua muda mrefu kuwa nje tofauti na matarajio yetu, tunaendelea kuliweka sawa hili lakini kesho utaona nani anacheza nafasi hiyo kwani wapo wengi wenye uwezo wa kucheza hapo.”

Kwa niaba ya wachezaji wetu, kipa Metacha Mnata, alisema: “Tunamshukuru Mungu tumefika salama, kwa sisi wachezaji tumejiandaa vizuri na tupo tayari kwa mchezo wa kesho, najua kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo huo, kwa hiyo tutajitahidi kadiri ya uwezo kwenda kupambana kuhakikisha tunapata pointi tatu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: