Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tunawaheshimu Mtibwa ila kesho watusamehe

Gamondi Bacca 6972d12 Gamondi: Tunawaheshimu Mtibwa ila kesho watusamehe

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa kesho Jumamosi timu ya Yanga SC itaikaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, kocha mkuu wa kikosi chetu, Miguel Gamondi ameuzungumzia mchezo huo.

Gamondi amesema kuelekea mchezo huo, amekiandaa vizuri kikosi chake kuibuka na ushindi, lakini kubwa zaidi wataingia uwanjani wakiwaheshimu wapinzani wetu, Mtibwa Sugar.

Mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 jioni, utakuwa wa kumi kwa timu yetu yenye pointi 24 kwa sasa baada ya kushuka dimbani mara tisa kunako Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

“Tumejiandaa vizuri, tulikuwa na wiki nzuri sana ya kujiweka sawa baada ya safari ndefu ya Ghana, kama unavyofahamu tuna wachezaji baadhi wana adhabu, majeruhi, lakini kesho tutajaribu kila liwezekanalo kushinda.

“Tunawaheshimu wapinzani, tunapaswa kufikiria kuhusu mchezo wa kesho, lakini katika akili yangu najua Jumatano tutakuwa na mchezo mwingine mgumu pia (dhidi ya Medeama katika Ligi ya Mabingwa Afrika). Kwa hilo ninaweza kusema tuna furaha tumekuwa na wiki nzuri ambayo tumefanya mazoezi na kuiandaa vizuri timu,” alisema Gamondi.

Kwa upande wa kipa, Aboutwalib Mshery, kuelekea mchezo wa kesho amesema: “Nikiwa kama muakilishi wa wachezaji wenzangu, tumejiandaa vizuri kwa sababu tunahitaji pointi tatu katika mchezo huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa msimu huu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: