Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tunataka kumaliza ligi vizuri

Aziz Gamondi WA0011 Gamondi: Tunataka kumaliza ligi vizuri

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amesema katika mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons, wataingia uwanjani kuhakikisha wanamaliza msimu vizuri.

Young Africans ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu ikiwa ni mara ya tatu mfululizo na 30 kwa ujumla, itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar katika kuhitimisha msimu wa ligi hiyo.

“Jana ilikuwa siku ya mapumziko, leo tunafanya mazoezi, tutajiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa msimu kuendelea kufanya vizuri. Nitaangalia hali za wachezaji lakini kiuhalisia ninaufikiria zaidi mchezo wa Jumapili (Fainali ya FA dhidi ya Azam).

“Haiwezi kuwa rahisi kujiandaa na mchezo, nadhani kila timu inatamani kuwa katika nafasi yangu na kushangilia, lakini tunaifanya kazi yetu. Tunapoangalia mechi tano za mwisho za wapinzani tunafahamu uchezaji wao na kila kitu.

“Wakati kama huu katika msimu wachezaji wanafahamu kila kitu kuhusu mbinu, lakini siyo rahisi. Leo tutaangalia wachezaji ambao watakuwa tayari kwa sababu wakati mwingine wachezaji wanaweza kupata majeraha au kuumwa, baada ya hapo tutafanya uamuzi wa wachezaji 20 wa kesho.

“Mwanzo kabisa tunapaswa kuwaheshimu mashabiki wetu kwa kucheza asilimia mia kila mchezo, siku zote zimekuwa nikiwaambia wachezaji, hata kipindi hiki ambacho hatuna presha tunatakiwa kudhihirisha ubora wetu na kuwaonesha mashabiki na kuwaheshimu wapinzani.

“Ninawaheshimu wapinzani wote, siwezi kuzungumza vibaya. Nina bahati ya kufundisha timu kubwa kama Yanga na kila mtu anatamani kushinda anapocheza dhidi ya Yanga.

“Wachezaji nimekuwa nikiwaambia wanapaswa kucheza kwa kujitoa kwa asilimia mia moja, katika maisha yangu sitoi nafasi ya kuridhika katika kila hali, nataka kufanikiwa siku zote,” alisema Gamondi.

Katika hatua nyingine, Gamondi amewasifia wachezaji wake akisema: “Tuna bahati ya kuwa na kundi bora la wachezaji ambao ni waelewa na tunazungumza vizuri, tunataka kudhihirisha ubora wetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live