Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tunaenda kuwapa burudani Mashabiki wetu

Gamondi Press Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikijiandaa kuwavaa Singida Fountain Gate kesho Oktoba 27 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amewatoa hofu mashabiki akisema wamedhamiria kuwapa burudani Mashabiki wao.

Akizungumza katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari Gamondi amesema;

"Kesho tunakwenda kwenye mchezo mwingine mgumu dhidi ya Singida lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo na kuwapa burudani Mashabiki wetu wanaokuja kutupa nguvu kipindi chote cha mechi zetu tukiwa Uwanjani"

"Hautakuwa mchezo rahisi kwasababu kuna vitu vingi vimebadilika kwa mpinzani wetu Singida, wana benchi la ufundi jipya na lenye maarifa tofauti. Tutacheza kwa kujituma na kwa tahadhari kwasababu tunahitaji ushindi kwenye kila mchezo"

"Kwa kipekee kabisa napenda kuwashukuru Mashabiki wetu kwa kutushangilia kwa nguvu na kutusaidia kupata ushindi dhidi ya Azam kwa kutokea nyuma na nina imani kesho watajitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: