Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tumedhamiria kutoboa makundi

Gamondi Coastal Gamondi: Tumedhamiria kutoboa makundi

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanavuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kwenda hatua inayofuata ya robo fainali.

Gamondi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari nchini Ghana kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Medeama FC ya nchini humo huku akisisitiza kuwa, mchezo wa kesho lazima apate ushindi ili kufufua matumaini hayo.

“Tumejiandaa vizuri, licha ya kwamba hatujaanza vizuri kwenye mashindano haya, lakini tuna malengo ya kucheza mchezo mzuri kesho, kwetu sisi ni mchezo ambao ni lazima tushinde kama tunadhamiria kushinda kutoka hatua ya makundi.

“Tunajua mechi haitakuwa nyepesi, lakini tutafanya kila tuwezalo kupata alama tatu. Kama tuna alama moja tu, maana yake timu zote ziko vizuri. Tumefanya makossa kwenye michezo iliyopita, tumejifunza na kufanyia kazi pale tulipokosea.

“Sasa tupo kwenye maandalizi ya mwisho kuhakikisha tunapata alama tatu kwenye mchezo wa kesho licha ya kwamba utakuwa mchezo mgumu,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live