Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Tangu niwe kocha, sijawahi kuwa na wachezaji bora kama Yanga

Yanga Pacome Gamondi Zdc Kocha Gamondi

Sat, 18 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Timu ya Yanga SC, Miguel Gamondi amesema moja ya vitu anavyojivunia katika kikosi chake ni kuwa na wachezaji wenye kiu na njaa ya magoli kitu ambacho kinampa faida kwenye kupata matokeo uwanjani.

Akizungumza kuelekea mchezo wa kesho Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya IHEFU kocha huyo amesema haishangazi kuona wachezaji wengi wapo kwenye orodha za juu za wafungaji msimu huu.

"Tunaamini tuna kila sababu ya kuendelea kufanya vizuri msimu huu, tuna wachezaji wanaopenda kutafuta magoli na kufunga ndio maana wachezaji wetu wapo kwenye orodha ya wafungaji bora kwenye kila mashindano. Tangu nifundishe soka, sijawahi kuwa na kundi la wachezaji bora kama nilionao Yanga," amesema Gamondi

Kuhusu mchezo wa kesho kocha huyo amesema anachofikiria ni kutinga fainali ya michuano hiyo licha ya ukweli kwamba atakumbana na wapinzani wagumu lakini watapambana kwa ajili ya furaha kwa Wananchi.

"Maandalizi yanaendelea vizuri, tumepata muda mzuri wa maandalizi baada ya mechi yetu ya ligi, mchezo wa kesho ni mchezo mkubwa na hautakuwa mchezo rahisi lakini sisi ni washindani na tutahakikisha tunapambana kupata ushindi na kwenda fainali," amesema kocha huyo.

Hii ni kwa mara ya tatu timu hizo zinakutana msimu huu ambapo kila timu imeshinda mchezo mmoja, wakitangualia Ihefu kushinda mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu mkondo wa kwanza na kisha Yanga kushinda mabao 5-0 kwenye mchezo wa mkondo wa pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live