Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Siwezi kufanya rotation kama napata matokeo

Gamondi Musonda Mede Gamondi: Siwezi kufanya rotation kama napata matokeo

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema watu wengi wanahoji kwanini hatoi nafasi ya wachezaji wengine kupata nafasi kwenye kikosi chake ‘Rotation’ lakini yeye anajua kwanini anafanya hivyo.

Gamondi amesema watu wanaohoji jambo hilo ndio walewale waliozungumza siku alipofanya mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Ihefu mchezo ambao Yanga walitandikwa mabao 2-1 mkoani Mbeya.

"Nakumbuka mchezo dhidi ya Ihefu nilifanya ‘Rotation’ nikawapanga akina Diarra, Bakari, Kibwana Moloko, Skudu, Mzize na niwaambie tuu hawa ni wachezaji wakubwa sikupanga timu ya vijana lakini tulifungwa, hatukufungwa kwasababu ya ‘Rotation’ tulifungwa kwasababu hata msimu uliopita tulifungwa pia" amesema Gamondi.

Kocha huyo ameongeza kuwa haoni sababu ya kufanya mabadiliko ikiwa bado anaendelea kupata ushindi katika michezo ambayo anacheza na atafanya mabadiliko ikiwa yeye na benchi lake la ufundi wataona ipo haja ya kufanya hivyo.

Kesho Yanga watashuka dimbani kuwavaa Mtibwa Sugar kwenye muendelezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: