Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Simba, Yanga hakuna 'underdog'

Simba Yanga 2024 Gamondi: Simba, Yanga hakuna 'underdog'

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa sio jambo la msingi sana kwake kuwajua wachezaji wapya wa Simba Sc, badala yake ameelekeza nguvu na akili yake katika kuandaa kikosi chake kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho.

Gamondi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaopigwa katika Dimba la Mkapa majira ya saa 1:00.

"Mnanijua mimi ninamheshimu sana kila mpinzani wangu ninapokuwa nakutana naye, timu zote hizi mbili Simba na Yanga hakuna underdog, Simba wana kocha mpya, wachezaji wapya wanataka kumuonesha mwalimu wao kwamba wanaweza, watakuja na ari ya juu kama ambavyo sisi tutaingia kwenye mchezo huo.

"Mwanzoni mchezo huo utakuwa ni 50/50, wakati mwingine unasema ukishinda sio kwamba uko bora sana kuliko mwenzako lakini jambo la msingi ni kuhakikisha tunakuwa bora msimu mzima kwa mafanikio ya klabu yetu bila kujali tunacheza na nani.

"Sisi makocha tunaandaa wachezaji kwenye uwanja wa mazoezi, ikifika kwenye mechi linakuwa jukumu lao kufanyia kazi maelekezo yetu. Ninajua Simba wanacheza vizuri, itakuwa mechi ya kushambuliana kwa zamu lakini utakuwa mchezo mgumu sana.

"Siwezi kusema nini kitatokea lakini nitakachokifanya ni kuhakikisha tunamiliki mpira na kutengeneza nafasi ili tuzitumie kufunga mabao. Mechi iliyopita tulitenegeneza nafasi nyingi lakini tulitumia chache, wiki hii yote nimekuwa nikilifanyia kazi hilo kuhakikisha tunatumia nafasi vizuri na kurekebisha makosa kwenye safu ya ulinzi," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: