Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi amesema kuwa kabla ya mchezo wa jana kumalizika hakufikiria iwapo wangeifunga CR Belouizdad ya Algeria kwa bao 4-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Gamondi amesema hayo jana Jumamosi, Februari 24, 2024 baada ya kutamatika kwa mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad na kuwafunga bao 4-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao utapigwa weekendijayo.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo wa jana kutamatika, Mabingwa hao wa Algeria walikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa huo ikiwa ni pamoja na Al Ahly, Mamelodi Sundowns na Wydad Casablanca.
Ikumbukwe kuwa, katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizi mbili uliopigwa nchini Algeria, Yanga ilinyukwa bao 3-0, lakini Wananchi hawakupoteza malengo yao ya kuitaka robo fainali.
"Kabla ya mchezo huu wa leo mtu yoyote angeniuliza tungeshinda ngapi ningesema goli 1, ila nimeshangazwa na hamasa ya wachezaji wangu leo kumwa jasho jingi kuipigania Yanga. Kwangu nawashukuru sana kwa pamoja tumeweza kufikia malengo yetu," amesema Gamondi.