Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Sasa tukutane Zanzibar

Pacome Gamondi Maxi Kocha Gamondi

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufunga mwaka kwa kupata ushindi ugenini mbele ya Tabora United, kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema burudani sasa inahamia visiwani Zanzibar wakati Yanga itakapokwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza kesho kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Unguja.

Mashabiki wa soka wa Zanzibar wanatarajia kuiona ile shoo ya Maxi Nzengeli na Yao Kouassi wakati timu hiyo iliyopangwa Kundi C ikiwa sambamba na Jamhuri, KVZ na Jamus ya Sudan Kusini itakapoliamsha bila kuwa na wachezaji wengine wakali kama Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki walioitwa timu za taifa.

Kikosi cha Yanga kinachotarajia kushiriki Mapinduzi Cup kitakosa mastaa wengi wa kikosi cha kwanza hasa eneo la kipa ambalo lote limeitwa kwenye vikosi vyao vya timu ya taifa, hivyo ni wazi wataongozwa na kipa wa timu ya vijana.

Makipa wa Yanga Djgui Diarra, Metacha Mnata na Abuutwalib Mshary wote hawatakuwa sehemu ya kikosi cha mashindano hayo msimu huu huku wazawa wakianza na mchezo wa ufunguzi Uwanja wa Amaan unaochezwa leo Jumatano.

Mastaa wa Yanga watakaoiwakilisha timu kenye mashindano hayo ni Yao, Maxi, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Joyce Lomalisa, Kibwana Shomari, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Zawadi Mauya, Jonas Mkude, Denis Nkane, Farid Mussa na Mahlats Makudubela huku wengine wakitajwa kuwa watachukuliwa timu ya vijana.

Wakati mastaa watakao kosekana kutokana na kujumuishwa kwenye vikosi vya awali vya timu zao za taifa kupigania bendera za nchi zao kwenye michuano ya Afcon inayotarajia kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024.

Mastaa hao ni Diarra, Metacha, Mshery, Aziz Ki, Pacome, Gift Fred, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Nikson Kibabage, Mudathir Yahya, Kenneddy Musonda, Clement Mzize na Hafiz Konkoni.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema hakutakuwa na mapumziko kwa mchezaji yeyote ndani ya kikosi chake kwani bado wana safari ndefu ili kuhakikisha wanatetea taji la ligi na kufikia malengo katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itarejea tena mwezi Februari, mwakani.

“Siwezi kutoa mapumziko wakati baadhi ya wachezaji watakuwa wanaendelea walipoishia kutokana na kuwa na ratiba ngumu mara baada ya mashindano ya Mapinduzi na Afcon kuisha tunarudi kwenye ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika.” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live