Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Sasa Pacome yuko fiti, kesho atacheza

Gamondi Pacome Aziz Ms Gamondi: Pacome yuko fiti, kesho atacheza

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Pacome Zouzoua huenda akacheza kesho wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tabora United baada ya kurejea kwenye utimamu wake kutokana na mazoezi ambayo ameshafanya.

Gamondi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo ikiwa ni mwezi mzima umepita tangu Pacome alivyoumia kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Azam FC.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, mechi ya robo fainali siyo nyepesi, kwenye Ligi ni dakika 90 tu lakini mchezo huu wa robo fainali lazima mshindi apatikane. Tabora wametoka kushinda mchezo wa Ligi uliopita, tunawaheshimu Tabora lakini tupo nyumbani na tunataka ushindi ili kuelekea kutimiza malengo yetu msimu huu.

“Kuna uweezekano wa kumtumia Pacome Zaouzoua, ameshaanza kufanya mazoezi ya kawaida na wenzake, tutaona leo mchana nini kitatokea, lakini hata kama ikishindikana mechi hii ya kesho, tunaweza kumuona mechi ijayo angalau dakika 20, tutaona maendeleo yake leo mchana. Mabadiliko kiufundi tutaona hiyo kesho.

“Mora;li ya wachezaji iko juu, nimefurahi mazoezi ya jana kila mchezaji ana morali ya juu na shauku ya kupata ushindi. Uzuri wa kikosi change ni kipana na kina wachezaji wengi wazuri wanaocheza kwa umoja, wana njaa na hamu ya kutaka kucheza kila mechi na kushinda, tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho kwa mazingira yoyote,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live