Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Ningekuwa na Mayele ingekuwaje?

Hg Mayele Gamondi: Ningekuwa na Mayele ingekuwaje?

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewajibu baadhi ya mashabiki wanaomtala kocha huyo afanye rotation kwa wachezaji wake kama alivyokuwa akifanya mtangulizi wake, Nasreddine Nabi misimu miwili iliyopita.

Gamondi amesema baadhi ya wachezaji wake hampi anachokitaka hivyo analazimika kuwatumia wachezaji ambao angalau wanampatia mabao kwenye kila mchezo tofauti na baadhi ya mashabiki wanachokitaka.

"Msimu huu kikosi changu kimefunga mabao 40, 8 yamefungwa na Stephen Aziz KI, Maxi Nzengeli amefunga 8 na 7 amefunga Pacoume Zouzoua na nina washambuliaji watatu Afiz Konkon amefunga bao 1 na nakubali hajacheza vizuri tangu ajiunge na Yanga SC.

"Clement Mzize ana mabao 4 na Kennedy Musonda mabao 4, unataka nifanye nini kama Fiston Mayele amefunga magoli 30 msimu uliopita kama ningekuwa nae kwenye kikosi ingekuwaje?," amesems Kocha Yanga SC Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live