Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ametengeneza timu yenye uwiano na inayotegemeana kwa kila mchezaji ndiyo maana inaweza kupata matokeo mazuri na kuzuia kufungwa.
Gamondi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuekelea mchezo wake wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC utakaopigwa katika Dimba la Azam Complex, Cghamazi, Dar es Salaam.
"Nimejenga mazingira ya kuwa na timu iliyo na uwiano mzuri kwa kila idara, tazama tumefunga magoli mengi lakini vile vile tumeruhusu goli moja tu katika michezo saba tena bao la penati ambalo ilikuwa kosa letu.
"Sasa ili uwe na uwiano na namna hiyo lazima ujenge timu inayotegemeana na sio timu inayomtegemea mtu fulani kwenye idara fulani.
"Jambo ambalo nimezingatia kwanza ni wachezaji kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe, pili wachezaji kuheshimu falsafa zangu, huwezi kuwa kocha mzuri kama wachezaji hawakuheshimu. Kimsingi matokeo chanya ya sasa ni kutokana na jitihada za wachezaji na benchi la ufundi," amesema Gamondi.