Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Ni mchezo wa kwenda kuchukua alama tatu

Gamondi Ms Gamondi: Ni mchezo wa kwenda kuonyesha ukubwa wetu

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ihefu mpo? Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameahidi kuonesha kandanda safi na kuondoka na ushindi katika mchezo dhidi ya Ihefu utakaopigwa katika Uwanja wa Hinhland Estates Jijini Mbeya.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara hatua ya mzunguko wa nne unatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:oo Jioni.

Katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari, Kocha wa Yanga raia wa Argentina Miguel Gamondi amesema kuwa ushindi katika mchezo huo ndio lengo lao kuu na si vinginevyo.

Gamondi anasema;

"Tunafahamu kwamba ni mwanzo wa ligi na kila timu iko kwenye nafasi nzuri na kujaribu kufanya vizuri zaidi inapokutana na bingwa mtetezi, ni sisi sasa kuhakikisha tunaendelea kucheza kwa kiwango cha juu na nina imani tutaendelea kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: