Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Napenda mechi kama hii ya Azam

Gamondi Mshz Kocha Gamondi

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanatarajia mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao hususan katika eneo lao la ulinzi.

Gamondi ameongeza kuwa Yanga ni kikosi imara chenye wachezaji wenye vipaji vikubwa lakini amesisitiza kuwa kipaji pekee hakitoshi kushinda mchezo, wachezaji wanapaswa kujituma zaidi ili kushinda.

“Napenda kucheza aina hii ya mechi, tumecheza na Simba sasa Azam ni kipimo sahihi kuelekea msimu mpya, tumekuwa na mwendelezo mzuri tokea tumecheza fainali Zanzibar, napocheza na wapinzani wagumu basi unaimarisha zaidi kikosi chako kiushindani, nina matumaini kesho tutacheza vizuri.

“Tumetumia jitihada kubwa kwenye mchezo uliopita, sina wasiwasi na kikosi changu kwani nina kikosi kipana ambacho kinanipa uhuru wa kupanga wachezaji tofauti, nina jua kesho (leo) tutakuwa na mchezo mgumu sana lakini nina imani na vijana wangu.

“Huu ni mchezo wa fainali, unapaswa kuwa makini sana, nakumbuka vyema mchezo uliopita pale Zanzibar, tayari tunayo picha sahihi tunapaswa kwenda na mbinu gani dhidi ya Azam Fc, niwahakikishie Yanga Sc ni timu imara sana, ukitazama mchezo uliopita Simba walitengeneza nafasi moja tu kwa sababu tulikuwa imara kwenye kila idara ” amesema Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live