Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Namungo kama KMC tu!

Gamondi Metacha Gamondi na Metacha.

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa leo Ijumaa wa Ligi Kuu ya NBC kati ya timu ya Young Africans SC dhidi ya Namungo FC, Kocha Mkuu, Miguel Gamondi amesema namna timu alivyoiandaa.

Mchezo huo ni wa mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Young Africans iliibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mudathir Yahya.

“Tumejiandaa kama tunavyojiandaa mechi zingine, tuna shida kwa baadhi ya wachezaji, lakini naweza kusema kwamba kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kushinda kesho.

“Naweza kusema asante sana Wananchi kwa sababu ni watu wa tofauti sana kwa namna walivyotukaribisha na kila mkoa tunaoenda kuna msisimko mkubwa unaotupa nguvu ya kupambana na kucheza soka zuri.

“Ninaamini kesho (leo) watakuja na kutupa sapoti kwa maana ya kwamba kiukweli mchezo utakuwa mgumu sana, tunahitaji sapoti yao.

“Siku zote timu inapocheza na timu kubwa kama Yanga inakuwa na morali kubwa ya kuonesha, tunawaheshimu kwa sababu si rahisi kuwafunga Namungo, mechi ya iliyopita tuliwafunga dakika za mwishoni.

“Mchezo dhidi ya Namungo natarajia utakuwa sawa na uliopita (dhidi ya Namungo) ingawa kila mchezo ni tofauti, iwe kushinda au kufungwa hiyo inakupa morali ya kupambana. Utakuwa mchezo mzuri na ninaamini tutapata pointi tatu.”

Metacha Mnata akizungumza kwa niaba ya wachezaji alisema: “Tumejiandaa vizuri, tunasubiri kesho tuoneshe namna tulivyojiandaa, tunaomba sapoti ya mashabiki na wanachama wa Young Africans wajitokeze kwa wingi, tunajua uwepo wao ni mchango mkubwa kwetu kwani unatupa moyo tupambane zaidi na kuwapa furaha.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: