Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Najua KMC ni wagumu, lakini watapigwa

Gamondii Yanga Gamondi: Najua KMC ni wagumu, lakini watapigwa

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondia amesema kuwa kesho Agosti 23, 2023 anakwenda kuanza rasmi Ligi Kuu Tanzania Bara hivyo atahakikisha wachezaji wake wanapambana ili kupata matokeo na kuanza vizuri msimu mpya.

Gamondi ambaye ni msimu wake wa kwanza Tanzania, amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wake wa kesho dhidi ya KMC utakaopigwa katika Dimba la Azam Complex Chamazi, jijini Dar.

"Ratiba ni kweli ni ngumu kutokana na ratiba ya michezo kuwa mingi lakini hiyo ndio kazi yetu. Tunapaswa kujiandaa kama timu kubwa ili kupata matokeo chanya katika kila mechi.

"Tulikuwa na shida kwa Wachezaji kadhaa, tutawaangalia kwenye mazoezi ya leo mchana kuona kama tunaweza kuwatumia kesho. Lakini kiujumla afya za Wachezaji wetu ipo imara na wana utayari wa kucheza mchezo wa kesho.

"Ni mchezo wetu wa kwanza wa ligi na matarajio yetu ni kushinda,kwa timu kama Yanga kila mechi matarajio yetu ni ushindi. Tunafaham kuna upinzani mkubwa kutoka kwa KMC lakini kubwa zaidi kutoka kwetu ni kuanza vyema ili malengo yetu ya Ubingwa tuyaanze vyema.

"Nawasihi mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu wa kesho.

Tutacheza kandanda safi na la kuvutia ili tupate matokeo. Tupo kwenye njia sahihi, tumejipanga na tumejiandaa kuwapa burudani," amesema Kocha Gamondi.

Msimu uliopita, Yanga chini ya Kochga Nasreddine Nabi walimaliza wakiwa mabingwa wa Ligi Kuu, Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam, Ngao ya Jamii na walifanikiwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: