Kocha Miguel Gamondi alisema licha ya ubutu wa safu ya ushambuliaji ila hana wasiwasi na hilo kutokana na aina ya soka analofundisha kwani kila mchezaji anatakiwa kufunga bila kujali nafasi anayoicheza.
“Soka ninalofundisha ni la kushambulia na kukaba hivyo kila mchezaji uwanjani anatakiwa kufanya kazi bila kumwangalia nani anatakiwa kufanya nini, washambuliaji pia wanatakiwa kusaidia kukaba pale inapohitajika;
“Sifurahishwi na idadi ndogo ya mabao kutokana na nafasi nyingi zinazotengenezwa lakini hili halinifanyi kuamini kikosi changu kina mapungufu kwa sababu kwenye mechi nne imefunga mabao matano ambao sio wastani mbaya.”