Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Mpaka sasa mambo yako 'fresh'

Gamondi Pacome Aziz Ms Gamondi: Mpaka sasa mambo yako 'fresh'

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amefunguka kuhusu anavyoutathimini yake kwa klabu yake kuelekea mwisho msimu huu akisema kuwa kwa upande wake mambo yanakwenda vizuri na wapo kwenye njia sahihi kuelekea ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

Yanga wanaongoza Ligi Kuu ya NBC wakiwa na alama 62 mbele ya Azam FC wenye alama 54 na Simba Sc wenye alama 47 wanashika nafasi ya tatu.

“Msimu bado haujaisha lakini mpaka sasa nimefurahi na nimeridhika, na kila mtu anafuraha. Tumevunja rekodi nyingi, tumecheza Klabu Bingwa, tumefuzu robo fainali ya Klabu Bingwa, tupo robo fainali ya Kombe la Shirikisho, tumemfunga Simba.

“Ninapenda kwenda polepole, hatua kwa hatua na mwisho wa msimu tutafanya tathimini,” amesema Kocha wa Yanga Miguel Gamondi alipoulizwa kuhusu anavyoutathimini msimu huu mpaka sasa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live