Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Mechi ya mwisho Sauzi niliwapiga Mamelodi

Gamondi Yanga Ms Gamondi: Mechi ya mwisho Sauzi niliwapiga Mamelodi

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa timu yake imekwenda Afrika Kusini kwa lengo moja tu la kutafuta ushindi na kufuzu kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na si vinginevyo.

Gamondi amesema hayo leo Alhamisi Machi 4, 2024 wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa kesho nchini humo.

"Mechi yangu ya mwisho hapa Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Loftus, nilikuwa Kocha wa Platinum Stars na tuliifunga Mamelodi magoli 2-1. Nina heshima kubwa na Nchi hii, nimeishi vizuri na watu wa hapa Lakini kwa sasa nimerudi na Young Africans SC na tunataka kuwafurahisha watu wa Watanzania," amesema Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live