Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Mchezo wa kesho nina faida kuliko Fadlu

Fadlu Gamondi Gamondi: Mchezo wa kesho nina faida kuliko Fadlu

Wed, 7 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa sio jambo la msingi sana kwake kuwajua wachezaji wapya wa Simba Sc, badala yake ameelekeza nguvu na akili yake katika kuandaa kikosi chake kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho.

Gamondi amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaopigwa katika Dimba la Mkapa majira ya saa 1:00.

"Mimi nimefanya kazi na wachezaji wangu hawa mwaka mzima sasa licha ya kwamba tumeongeza wachezaji wengine kama saba, lakini kwa Fadlu ni kocha mpya, kikosi kipya na anaanza na mechi ya Dabi, analazimika kuwasoma wachezaji wake wote mpaka awajue mmoja mmoja.

"Hii inaweza kuwa faida kwangu lakini hii haimanishi kwamba ni sababu ya sisi kushinda mchezo huo. Soka ni mchezo wa makosa, na wakati mwingine mashabiki huwa hawaelewi, wao wanachokitaka ni matokeo tu," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: