Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Matokeo hayakuwa muhimu kwetu, ninachokipika mtakiona

Gamondi Chama Aziz Pacome Gamondi: Matokeo hayakuwa muhimu kwetu, ninachokipika mtakiona

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamond Raia wa Argentina baada ya timu yake kupoteza 2-1 dhidi ya Augsburg ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundlesliga) amehojiwa na SABC TV na kutoa maoni yake kuhusu kiwango cha timu yake.

“Kwetu tumeupokea vizuri huu mchezo kwa sababu usisahau tumecheza na timu ya kiwango cha juu sana, hii timu huwa inacheza dhidi ya Bayern Munich, Leverkusen na Dortmund kwetu sisi ndio kwanza tunaanza maandalizi na nimeona tumekuwa tunapoteza mipira kirahisi lakini ni kawaida kwa hatua hii ya maandalizi”

“Kwa ujumla nimeridhishwa na viwango vya Wachezaji wangu, kipindi cha kwanza walipoteza (Augsburg) nafasi mbili tatu na sisi tulipoteza nafasi mbili tatu na kipindi cha pili tulitawala na kutengeneza nafasi ambazo tungeweza kusawazisha hata dakika za mwisho.

“Wachezaji wangu wajitoa kila kitu, wamepambana sana kiufundi wamejitahidi, wameipambani nembo ya Yanga kama nilivyosema mwanzo, matokeo hayakuwa muhimu sana kwangu kwenye mchezo huu lakini cha muhimu ilikuwa ni jinsi gani timu inavyocheza.

“Tumecheza kwa kuwakabili, hatukuwaogopa na ninadhani tumeonesha ukubwa wetu Afrika kwa kucheza na miongoni mwa timu kubwa barani Ulaya,” amesema Gamondi.

Yanga SC bado wataendelea kusalia Afrika Kusini hadi July 28 watakapocheza mchezo wao wa pili wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live