Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Mashabiki tulieni, hesabu ziko sawa

Pacome Gamondi Maxi Gamondi: Mashabiki tulieni, hesabu ziko sawa

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imerudi nchini ikitokea Ghana na mastaa wa timu hiyo leo wanarudi kambini kujiandaa na mechi mbili za ndani, huku kocha Miguel Gamondi akituliza presha kwa kuwaambia mashabiki kwamba watulie kwani hesabu bado ziko sawa.

“Kitu muhimu sasa ni kujipanga vizuri tuna mechi tatu ambazo lazima tubadilishe mambo ili hesabu zizidi kuwa kwetu najivunia wachezaji wangu na hata mashabiki wetu hasa hizi mechi mbili za nyumbani kabla ya kwenda kumalizia ugenini, lazima tujitoea kwa kiwango kikubwa.”

“Tutarudi kambini leo kuanza maandalizi ya mechi mbili za ndani mojo ya FA na nyingine ya ligi, ni wakati muafaka sasa kuelekeza akili zetu kwenye michezo hiyo muhimu kabla ya kuanza kuangalia mechi za Afrika,” alisema Gamondi.

Yanga itacheza na Haulung ya Njombe Disemba 13 mechi ya ASFC kisha kuivaa Mtibwa katika Ligi siku tatu baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: