Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Mambo ni mengi mda ni mchache

Aziz Gamondi WA0011 Miguel Gamondi.

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi amesema licha ya kwamba hakuna muda mwingi wa maandalizi, lakini anachokifanya na wenzake wa benchi la ufundi ni kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika kusaka ushindi ikiwemo kuangalia video za wapinzani.

Kauli ya Gamondi imekuja kuelekea mchezo wa leo Jumatano wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Young Africans itaingia kwenye mchezo huo ikitoka kushinda ugenini mkoani Kigoma goli 1-0 dhidi ya Mashujaa, Jumapili iliyopita.

“Muda wa maandalizi ni mdogo, tunachokifanya ni kuifanyia tathmini Kagera Sugar kupitia video zao na leo tunamalizia mambo yote ya maandalizi ikiwemo kuwaangalia wachezaji wenye majeraha na utimamu wa waliocheza mechi ya Jumapili.

“Lakini tunaamini tupo tayari kwa mchezo wa kesho na kupata pointi tatu katika hatua ya mwisho ya msimu.

“Kila mechi ni ngumu, ukiangalia mechi zetu tano za mwisho hazikuwa rahisi , Kagera ni wapinzani wazuri, walitupa ugumu, kesho tuna faida ya kucheza nyumbani Chamazi.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera, matokeo yalikuwa 0-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live