Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ni lazima afanye rotation kwa wachezaji wake ili kuwapa nafasi wachezaji wote ili timu iweze kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.
Gamondi amesema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la NBC dhidi ya Tabora United na kufanikiwa kushinda bao 3-0 katika Dimba la Chamazi
“Ninafuraha kwa kufanikiwa kufuzu kwenda nusu fainali, kiwango kizuri hata kipindi cha kwanza nilikuwa na furaha sana, tulitembeza mpira haraka haraka kama ambavyo tulipanga kufanya. Tlitawala mchezo na kutenegeza nafasi lakini tulitumia moja tukapata bao na hata kipindi cha pili tulikuwa vizuri.
“Kwenye mechi nane za mwisho tumeruhusu bao moja tu dhidi ya Simba, ni jambo zuri hasa mwisho wa msimu.
“Tuna timu kubwa lazima tufanye rotation. Mwezi uliopita tulicheza mechi 7, mwezi huu tuna mechi nane, hawezi akacheza mchezaji yule yule kila mechi, kuna kusafiri, kuchoka, lazima apumzike acheze mwingine ili kutunza nguvu, majeraha kwa hiyo tunalazimika kufanya hivyo ili kukilinda kikosi chetu,” amesema Gamondi.
Pamoja na majeruhi, katika mchezo wa jana Gamondi aliwapumzisha nyota wake kama Dickson Job, Kouassi Yao, Augustine Okrah na wengine.