Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Kwa mziki huu wewe huogopi!

Miguel Gamondi Semi Final Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ametambia mastaa wake Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli kuelekea mchezo wa hatua nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), huku akisisitiza kwamba wanataka kutinga hatua inayofuata.

Yanga inashuka dimbani ikiwa tayari imetawazwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu ikisaka taji la pili dhidi ya Ihefu FC kwenye mchezo huo utakaochezwa saa 9:30 alasiri katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

"Nina mchezaji ambaye ni mfungaji bora wa ligi kwa kufunga mabao mengi. Nina mchezaji ambaye pia ni mzuri kwenye kutoa pasi za mwisho (asisti), nina Pacome na Maxi bado niwe na wasiwasi?" amehoji na kuongeza:

"Sina hofu yoyote najivunia kikosi changu. Nina timu ambayo inacheza kimbinu na imekuwa ikishirikiana kwenye kila kitu. Sitegemei mabeki kwenye kukaba timu nzima inafanya hivyo na kushambulia wanakiwa pamoja."

Amesema kesho anachotaka ni ushindi na sio kitu kingine, huku akisisitita kuwa timu yenye wachezaji bora ndio itaamua mchezo huo ndani ya dakika 90 akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kushuhudia boli litakavyotembea na mabao yatakayofungwa.

Hata hivyo, wakati Gamondi akitambia kikosi bora, Kocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema kikosi chake kipo tayari kwa asilimia 80 kukabiliana na Yanga akisistiza kuimarika na kuwa bora zaidi kitakachoonyesha ushindani katika mcheso huo.

"Nafasi kubwa wanapewa Yanga kwa sababu wametoka kutwaa taji la ligi. Ni kweli wana kikosi bora, lakini wanatakiwa kufahamu pia kuwa na sisi tumeimarika na timu imepata muunganiko mzuri," amesema.

"Yanga wapo vizuri na wana wachezaji wa kuamua mchezo kama alivyosema kocha wao na sisi pia tupo vizuri. Ili kuweza kukabiliana na timu hiyo tunatakiwa kwenda na kasi yao. Wao wanakimbia sana ukiwaacha wanakuadhibu, sisi pia tunatakiwa kukimbia zaidi yao ili tupate matokeo."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: