Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Kwa Geita tutaingia kivingine, wasitukariri!

Gamondi Yanga Ms Gamondi na wachezaji wake.

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Angel Miguel Gamondi amesema kuwa kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kupambana na Geita Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa kesho katika Dimba la Chamazi.

Akizungumza leo kwenye mkutano na wanahabari, Gamondi amesema kuwa siku zote amekuwa akibadilisha mbinu na falsafa kulingana na mpinzani anayekutana naye, hivyo kulingana na ubora walio nao Gaita kwa sasa, ameandaa mbinu bora ya kuwakabili ili kupata matokeo chanya.

"Tumejiandaa vizuri kucheza na Geita Gold, tunafahamu kila mpinzani kuna namna yake ya kujiandaa kimbinu, Ukitazama matokeo yao ya hivi karibuni wameimarika hivyo lazima tuchukue tahadhari ya kutosha bila kujali matokeo yetu ya awali”

“Nina wachezaji wengi wazuri sana, tunaweza kucheza aina yoyote ya mchezo, iwe kushambulia, kumiliki mpira nk. Tunaweza kubadilika badilika kulingana na matakwa ya mchezo kabla na wakati wa mchezo, sijawahi kucheza na aina moja ya falsafa huwa nabadilika kulingana na namna mpinzani anavyocheza na namna navyoweza kumkabili.

“Mechi tano tumefunga magoli 15, tumeruhusu bao 3, kimsingi hizi ni takwimu bora siwezi kusema kwamba Geita nao tutawafunga magoli mengi huo utakuwa ubashiri sifanyi kazi ya kubashiri, ninachoweza kufanya kwa sasa ni kujiandaa kushinda mchezo.

“Tumejiandaa kucheza nao kwa namna yoyote ambayo watajipanga, nafikiri watakuja na mbinu za kujilinda lakini hainipi hofu kwa sababu nina vijana wazuri,” amesema Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live