Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Kurejea kwa Pacome 'good news' kwa mashabiki

Pacome Zcss Pacome Zouzoua.

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa kurejea kwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Pacome Zouzoua ni taarifa njema kwake na mashabiki wa Yanga kwani mchezaji huyo ni muhimu ndani ya kikosi hicho.

Pacome alirejea dimbani jana baada ya kukaa nje kwa takribani mwezi mzima na nusu kufuatia majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Azam FC na jana akafanikiwa kutoa assist ya bao.

“Ninafuraha kwa kufanikiwa kufuzu kwenda nusu fainali, kiwango kizuri hata kipindi cha kwanza nilikuwa na furaha sana, tulitembeza mpira haraka haraka kama ambavyo tulipanga kufanya. Tlitawala mchezo na kutenegeza nafasi lakini tulitumia moja tukapata bao na hata kipindi cha pili tulikuwa vizuri.

“Kurejea kwa Pacome ni good news kwetu na tumemuona amekuja kwenye kiwango kizuri licha ya kukaa nje kwa zaidi ya mwezi mzima lakini amecheza vizuri kutokana na uwezo wake mkubwa, nadhani hata Wananchi wanatakiwa kuwa na furaha kwa hilo.

“Tutaendelea kumpa nafasi polepole arejee kwenye kiwango chake halisi. Jana nimempa dakika 25, mchezo ujao nitampa dakika nyingine polepole mpaka awe fit. Siwezi kumpa dakika 90 kwa sasa kwa sababu bado hayuko fiti,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live