Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Kesho hatutashambulia hovyohovyo

Gamondi Bacca 6972d12 Kocha Gamondi.

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondia mesema kuwa makosa ya kiulinzi waliyoyafanya wakati wa mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad nchini Algeria hawatayarudia tena kwenye mchezo wa kesho.

Gamondi amesema hayo leo wakati wa mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Belouizdad utakaopigwa katika Dimba la benjamin Mkapa, Dar.

“Kwetu sisi ni mchezo muhimu na mchezo ambao ni lazima tushinde. Tupo kwenye kundi gumu na tuko na timu ambazo zina uzoefu mkubwa lakini tunajua na sisi tuna timu nzuri. Tunacheza nyumbani.

“Tumetoka kucheza mechi ya FA, maandalizi yetu ni mazuri licha ya kupata muda mchache wa maandalizi kuelekea mchezo wetu wa kesho, lakini tumejiandaa kutoa kila kitu kwa mashabiki zetu Wananchi ili kushinda mchezo wetu.

“Tunafahamu tulifanya makossa kwenye mchezo uliopita CR Belouizdad wakatuadhibu kwao, ni wazuri kwenye mashambulizi ya kushitukiza hasa kupitia pembeni, hilo tumeshalifanyia kazi hatutashambulia hovyohovyo lazima tuwe makini wakati wa kushambulia na kukaba.

“Tumejiandaa kisaikolojia, wachezaji wapo tayari kupambana kwenye mchezo wa kesho, hautakuwa mchezo rahisi. Tutacheza kwa umakini mkubwa tunajua mashabiki watajitokeza kuisapoti timu yetu tupate ushindi, uwanja utajaa,” amesema Gamondi.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga walikubali kupokea kipigo cha bao 3-0 kutoka kwa CR Belouizdad, hivyo kesho ni mchezo muhimu kwao na endapo watashinda basi watakuwa wamejiwekea mazingira mazuri ya kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: