Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: JKT ni wazuri lakini sisi tunataka ushindi

Fdv Guede Gamondi Mzs Gamondi: JKT ni wazuri lakini sisi tunataka ushindi

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea kwenye mchezo wa kesho JKT Tanzania dhidi ya Yanga Africas, Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema hawawezi kuzungumzia sana maandalizi kwa sababu Jumamosi wametoka kucheza mechi.

Gamondi amesema kazi kubwa amehakikisha wamefanya mazoezi ya kujiweka sawa hivyo kwa sasa wanacheza ili washinde mchezo na hawezi kuahidi idadi ya magoli atakayoshinda kikubwa wanachotaka alama tatu.

Gamondi amesema mechi dhidi ya JKT itakuwa ya ushindani mkubwa kwa sababu utakuwa mchezo mwingine na anaimani wapinzani wake watakuja kivingine tofauti na walipokutana mechi ya mzunguko wa kwanza.

“Ninawaheshimu JK wana timu nzuri, wanakaba sana kwa hiyo kuwafungua ni kazi ngumu, kwenye mechi tano za mwisho wameruhusu bao moja tu, lakini sisi tunataka ushindi. Hatujafanya mazoezi sana kutokana na kwamba mechi ya juzi ilikuwa ngumu.

“Jambo kubwa lilikuwa ni recovering kwa hiyo tutaangalia wachezaji fresh ili kupata matokeo. Tunatengeneza nafasi nyingi sana hivyo ni jukumu la wachezaji kuzitumia kufunga mabao. Sijui hali ya uwanja ikoje, lakini tutaenda kuona huko huko,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live