Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Ihefu walitujeruhi, leo tutalipa kisasi

Gamondi Bacca 6972d12 Gamondi: Ihefu walitujeruhi, leo tutalipa kisasi

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua ambaye alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Namungo 1-3 Yanga, Joseph Guede na mdaka mishale Djigui Diarra wamerejea kwenye uwanja wa mazoezi.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema walijeruhiwa mchezo wa mzunguko wa kwanza wanakwenda kucheza kwa umakini kupata pointi tatu.

"Tulijeruhiwa na Ihefu mchezo wa mzunguko wa kwanza, wachezaji wetu wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu mashabiki wajitokeze kupata burudani,'.

"Kwetu kila mechi ni muhimu na tunataka kushinda hivyo leo tunakwenda kufanya mazoezi ya mwisho ili kuwapa furaha wananchi”

“Tunajua Ihefu ndiyo timu pekee iliyotujeruhi msimu huu na kesho Ileo) ni siku nzuri ya kulipiza kisasi hiki, wachezaji wanafahamu, benchi la ufundi tunafahamu na tunaamini tutapata alama tatu kesho.

"Binafsi sikufurahi kabisa tulivyocheza mchezo wetu dhidi ya Ihefu najua pia Wananchi hawakufurahi hivyo nawaomba kesho wajitokeze kwa wingi kwakuwa wachezaji wanatambua kuwa wao ndiyo mchezaji wa 12, waje kwa wingi kushuhudia burudani nzuri na tukipamba kupata alama tatu muhimu,” amesema Kocha Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live