Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hii Mechi sio ngumu, lazima tushinde

Hersi X Gamondi Usajili Gamondi: Hii Mechi sio ngumu, lazima tushinde

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga Miguel Angel Gamondi amesema mchezo wa kesho dhidi ya Medeama lazima wapate ushindi kwasababu mchezo huo sio mgumu sana.

Gamondi pia amewataka wachezaji kujituma ili kuwapa furaha mashabiki lakini pia wawe makini na wajitoe kwaajili ya kuhakikisha timu inapata matokeo.

"Ni mechi ya lazima kushinda kesho, sio ngumu sana kwasababu hata mashabiki wetu wanajua kuanzia mwanzo kuwa tunapaswa kushinda mchezo wetu wa kesho.

Wachezaji wetu wanapaswa kuwa makini na kujitoa kwa ajili ya ushindi, na uzuri tunajua namna ya kushinda".

Amesema Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi.

Gamondi atakiongoza kikosi cha Yanga hapo kesho Jumatano kwenye mchezo wa nne wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya makundi.

Timu hizo zimekutana mara moja msimu huu na katika mchezo huo timu zote mbili zimetoshana nguvu na kutoka sare ya kufungana goli 1-1 nchini Ghana.

Huu ni mchezo mwingine ambao Yanga inapewa nafasi kubwa zaidi ya kupata matokeo, ikumbukwe Medeama pia sio timu ya kubeza kwani iliifunga CR Belouizdad ambayo ilimfunga Yanga katika mchezo wa kwanza wa hatua hii.

Hadi hivi sana Yanga haijapata ushindi wa aina yoyote kwenye hatua hii, imecheza michezo mitatu (3) imetoa sare michezo miwili [2] na imepoteza mchezo mmoja (1), ipo nafasi ya mwisho ya msimamo wa kundi D.

Medeama wao wamecheza michezo mitatu (3), wameshinda mchezo mmoja (1), wamepoteza mchezo mmoja (1) na wametoa sare mchezo mmoja [1] ipo nafasi ya tatu (3) na alama zake nne (4).

Mshindi katika mchezo huu atajiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali.Kama Yanga itashinda itafikisha alama tano zitakazompeleka hadi nafasi ya pili au kuongoza kundi kutegemea na magoli itakayofunga.

Kama Medeama ataibuka na ushindi wa aina yoyote hii leo atafikisha alama saba (7) na itaongoza kundi D.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: