Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hesabu za ubingwa Yanga hazijakaa sawa

Miguel Gamondi Maboa Kesho Kocha Gamondi.

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa licha ya kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 8 lakini anaamini Yanga bado sio Bingwa mpaka pale mahesabu ya alama kikanuni yatakapokamilika.

Gamondi amesema hayo leo akijibu swali la mwandishi kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera ambapo amedai kuwa utakuwa mchezo mgumu hasa ikikumbukwa kuwa Kagera ndiyo timu ya kwanza msimu huu kutoa sare na Yanga katika mzunguko wa kwanza.

“Mimi kama Kocha na wachezaji wangu tunajua kwamba mpaka sasa Yanga sio Bingwa, tutakuwa mabingwa wakati ambao kimahesabu tutakuwa na alama ambazo zinaweza kutupa ubingwa, tunaziheshimu timu zote.

“Timu iliyoko nafasi ya pili na hata ya tatu zinapambana, hazijapoteza matumanini kwenye ligi. Ni kweli tuna gape kubwa la alama 8 na keshokutwa watacheza ambapo wenyewe kwa wenyewe, tutaona kama watatoa sare au mmoja wao atatoa gape zaidi kwetu lakini tunajikita na mechi yetu ya kesho ili kushinda.

“Falsafa yangu ni hatua kwa hatua, mechi kwa mechi, ninatengeneza shauku ya ushindi kwa kila mchezo na mechi hizi za mwisho ni ngumu sana, zipo timu zinajipapatua kujinusuru kushuka daraja na zipo zinatotaka nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika na ratiba ni ngumu kwetu sote, kucheza, kufanya recovery, kucheza tena,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live