Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hatutawachukulia poa JKT, kipigo kitaendelea

Yangasc 36 Gamondi Gamondi: Hatutawachukulia poa JKT, kipigo kitaendelea

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa hatawachukulia poa Klabu ya JKT Tanzania kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya timu hiyo kupanda daraja msimu huu.

Gamondi amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 28, 2023 kuelekea mchezo wao wa kesho wa ligi dhidi ya JKT Tanzania huku akiongeza kuwa falsafa yake ya kucheza soka la burudani itaendelea kama kawaida ikiwa timu yake imetoka kushinda bao 10 kwenye mechi mbili.

“Licha ya kwamba mpinzani wetu tunajua ni timu iliyopanda daraja, najua kwamba wana wachezaji wenye uzoefu kwenye ligi hivyo hatupaswi kuichukulia kama timu dhaifu au ngeni kwenye ligi.

“Ni wageni kwa maana ya timu lakini wana idadi kubwa ya wachezaji wenye uwezo lakini sisi ni timu kubwa na tupo nyuma nafikiri kesho tunapaswa kujiamini na kufunga magoli mengi.

“Nina heshimu kila mpinzani ambaye tunakutana nae, falsafa yangu ni kucheza mchezo mzuri bila kujali tunacheza na nani, lengo letu kubwa ni matokeo pamoja na furaha kwa Wananchi," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live