Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hatutapaki basi kwa Medeama

Gamondi Coastal Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimewasili nchini Ghana tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kucheza mchezo wao wa tatu muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi lakini kocha wao Miguel Gamondi akashusha mkwara mzito.

Akizungumza na Mwanaspoti Gamondi alisema wanakwenda kwenye mchezo huo wakiupa sura ya sawa na fainali katika kupigania malengo yao.

Gamondi alisema ingawa wamepata siku moja pekee ya maandalizi baada ya mchezo wao wa mwisho nyumbani dhidi ya Al Ahly ya Misri wakifungana bao 1-1 Sasa wanazitaka alama tatu.

Gamondi alisema kikosi chake hakitakwenda kupaki basi wala kujiachia lakini wanataka kucheza kwa nidhamu kubwa huku kitu muhimu wanatakiwa kuonyesha mabadiliko kwa kufunga mabao.

“Hakuna mechi rahisi kila mchezo ni mgumu hasa unapocheza ugenini, tumekuwa na siku moja pekee ya maandalizi kuelekea mechi hii ya ugenini ila hii sio sababu tunatakiwa kupambana,”alisema Gamondi ambaye bado anausaka ushindi wa kwanza kwenye hatua ya makundi.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu ni timu ambayo inaundwa na wachezaji bora, kwetu sisi hatuna nafasi ya kusema twende tukajilinde lakini kitu muhimu ni kucheza kwa nidhamu kubwa.

“Tukizuia vizuri na kisha kutumia nafasi za kufunga nafikiri tunaweza kupata matokeo ambayo tunayatafuta ni suala la kila mchezaji kutambua umuhimu wa ushindi kwa nafasi ambayo tupo sasa.

Yanga inahitaji kufufua matumaini yake kufuzu hatua ya robo fainali ambapo nafasi pekee ya kuanza kuelekea hesabu zao hizo ni kuhitaji kuifunga Medeama ambao tayari wa ushindi mmoja baada kuwachapa CR Belouizdad ya Algeria kwa mabao 2-1.

Mabosi wacheza hesabu za kikubwa

Yanga jana ilipotua Accra mabosi wao walishashtuka mchezo huo kupelekwa Jiji la Kumasi na kama safari hiyo wangetumia Basi wachezaji wao watachoka.

Wakakodisha ndege maalum ambayo ilibeba timu hiyo kutoka Accra kwenda Kumasi.

Kwa ndege hiyo, Yanga ilitumia muda wa dakika 35-60 pekee kufika Kumasi hesabu ambazo ziliwapunguzia uchovu ambapo kama wangetumia Barabara wangekaa masaa yasiyopungua manne kusafiri kilomita 202.

Yanga imechukua hoteli ya kisasa ya Ridge Condos yenye hadhi ya nyota 4.4 ambayo ndio hoteli ambayo inatumiwa na timu mbalimbali kubwa zinazofika jijini hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: