Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hatuna presha na Simba, tuko tayari kwa mapambano

Fd Nzengeli Gamondi Kocha Gamondi.

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi ameuzungumzia mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC tutakaocheza Novemba 5, 2023 dhidi ya Simba, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 11:00 jioni.

Gamondi amesema, vijana wake kwa asilimia 100 wapo tayari kwa ajili ya dabi hiyo ya Kariakoo, huku akiwataka mashabiki kuja kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji kuhakikisha pointi tatu zinakuwa zetu.

“Natambua ni mchezo mgumu na ni muhimu sana kwetu, lakini hatutakiwi kujiweka kwenye presha kubwa.

“Sisi tunaendelea na maandalizi yetu na mashabiki pia wajiandae na jukumu lao la kuja uwanjani kuwashangilia wachezaji wao.

“Kitu ninachoweza kuwahakikishia kwa asilimia 100 wachezaji wako tayari kwenda kupambana kupata pointi tatu kwenye dabi.”

Yanga wataingia kwenye mchezo huo wakiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ambapo wanahitaji ushindi ili kuendelea kusalia kileleni na kusafisha zaidi njia ya kutetea ubingwa wa ligi hiyo walioubeba mara mbili mfululizo msimu uliopita 2021-2022 na 2022-2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: