Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hao Tanzania Prisons tutajua huko huko

Pacome Gamondi Maxi Gamondi: Hao Tanzania Prisons tutajua huko huko

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa, amesema kuwa uchovu wa wachezaji na ubovu wa Uwanja wa Sokoine Mbeya unaweza kuufanya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons ukawa mgumu.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mashujaa FC huku Yanga ikionekana kusua sua kupata matokeo katika michezo yake mitatu iliyocheza ikitoa sare moja na kushinda miwili, ikifunga mabao matatu na kufungwa bao 1.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1, dakika za lala salama.

"Tunajua mechi dhidi ya Tanzania Prisons itakuwa ngumu. Tunafahamu uwanja sio rafiki, wachezaji wana uchovu kutokana na mechi mfululizo lakini tutapambana.

"Ratiba yetu tutaondoka kesho mapema, tutafanya recovering, jambo la mhimu ni kwenda kupambana, ku-enjoy soka na kupata alama tatu, hao Tanzania Prisons nitaanza kuwafikiria kesho," amesema Kocha Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live