Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Hakuna ugumu wa kupanga kikosi

Sac Gamondi Chama Dube Aziz Gamondi: Hakuna ugumu wa kupanga kikosi

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amekiangalia kikosi chake kuelekea msimu ujao kisha akasema hakuna ugumu wowote wa kukipanga siku ya mechi.

Gamondi ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na wanahabari Coco Beach wakati kikosi chake kikifanya mazoezi huku akijibu maswali ya wengi juu ya namna kikosi kitakavyopangwa baada ya usajili mkubwa na wenye malengo uliofanyika kipindi hiki.

Msimu ujao 2024-2025 Yanga watakuwa na mashindano ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC, CRDB Bank Federation Cup, Mapinduzi Cup na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kote huko malengo ni kufanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa 2023-2024.

“Hakuna ugumu kupanga kikosi cha Yanga kwa sasa, kila mchezo una mbinu zake hivyo kuna mchezo utacheza na viungo watatu kuna mchezo utaanza na Aziz Ki au Chama ama Pacome.

“Mastaa ni wengi lakini msisahau tuna mechi nyingi pia, hivyo kikosi kitatokana na mpinzani tunayekwenda kucheza naye,” alisema Gamondi.

Wachezaji wapya ndani ya kikosi mpaka sasa ni Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, mshambuliaji Prince Dube, beki wa kushoto Chadrack Boka, kipa Khumeiny Aboubakar na kiungo mkabaji Aziz Andambwile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live