Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Habari za ubingwa tumeweka pembeni, tunakwenda kupamabana na Kagera

Tu Gamondi Zs Gamondi: Habari za ubingwa tumeweka pembeni, tunakwenda kupamabana na Kagera

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ameweka pembeni habari za ubingwa wa msimu uliopita na anachokifanya sasa ni kuandaa mpango wa kufanikisha malengo yao msimu huu.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na Yanga TV kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Alhamisi, Agosti 29, 2024 katika Dimba la Kaitaba Bukoba.

“Kuna wakati kuna hivi vitu hutokea kwenye soka, hata kama una timu nzuri unaweza kupata matokeo mabaya. Kwangu mimi sitazami yam waka jana, ninaangalia nini tunakwenda kukifanya msimu huu. Msimu uliopita ni kama tulipoteza pale ninakumbuka vizuri huu mchezo.

“Kwa sasa ni tofauti kidogo, tunaijua Kagera namna inavyocheza na kikosi chetu kilivyo na tutakwenda kwa ajili ya kushinda, tupo tayari kupambana na tunachotaka ni matokeo. Ninajua uwanja sio rafiki pale, na timu hizi sio Kagera tu bali timu zote zinapocheza na Yanga zinakuja kupambana na kujaribu kutuzuia kwa sababu ni kama mchezo wa msimu kwao.

“Hatufikirii kama sisi ni mabingwa watetezi, tunapaswa kutulia na kuuendea mchezo kwa umakini. Kila mchezo lazima tuoneshe ukubwa na ubora wetu, ninaamini tutapata alama tatu,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live