Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Guede ninayemjua sasa kaanza kunoga

Fdv Guede Gamondi Mzs Gamondi na Guede.

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mshambuliaji wa Yanga SC, Joseph Guede kuonesha kiwango kizuri katika pambano la timu yake dhidi ya Singida Fountain Gate, kocha wa Yanga SC Miguel Gamondi, amesema nyota huyo ni mchezaji mahiri, lakini alihitaji muda.

Guede ambaye ni raia wa Ivory Coast alifunga mabao mawili kati ya matatu kwenye mchezo huo uliopigwa jana katika Dimba la CCM kirumba, jijini Mwanza.

“Ninamfahamu Guede tangu akiwa Morocco, ni mchezaji mzuri sana, hajanisapraizi kutokana na uwezo wake. Nimekuwa nikimpanga mara chache chache kwa sababu mara ya mwisho hakucheza sana.

“Ni mchezaji alikuwa anahitaji kupata nafasi ili kurejesha fitness na uwezo wake lakini pia kuingia kwenye mfumo ambao timu inacheza.

“Ninaamini huko mbeleni atakuja kuwa msaada mkubwa sana kwa Yanga na kwa soka la Tanzania,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live