Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Fainali ya Yanga na Azam itakuwa ya aina yake

Gamondi Yanga Ms Kocha Gamondi.

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzanbia Bara, Miguel Gamondi amesema kuwa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la NBC hautakuwa rahisi kutokana na mpinzani wao Azam FC kuwa na ubora kwenye msimu huu.

Yanga ambao pia ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho watakutana na Azam FC ambao ni washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu huu na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho msimu uliopita huku timu zote zikiwa zimefuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

“Ninadhani itakuwa fainali nzuri kwa sababu kwa siku za hivi karibuni Yanga na Azam zimeonesha kuwa ni timu bora kwenye nchi na Azam wamecheza vizuri sana, itakuwa fainali bora na yenye mvuto kwa soka la Tanzania.

“Waandaaji wamefanya vyema kupeleka mechi kwenye uwanja mzuri, itakuwa picha nzuri ya fainali bora kuwahi kuchezwa Tanzania na Afrika. Kila timu ina nafasi ya kushinda hiyo fainali,” amesema Gamondi.

Mchezo huo wa fainali itapigwa Jumapili ijayo Juni 2, 2024 katika Dimba la Amaan Visiwani Zanzbira, ambapo mwaka jana timu hizo zilikuwatana kwenye fainali ya kombe hilo iliyopigwa Mkwakwani Tanga na Yanga kufanikiwa kuibuka mabingwa wa ushindi wa bao 1 lililofungwa na Kennedy Musonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live