Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi: Dube na Baleke hawapo fit

Baleke Msz Gamondi: Dube na Baleke hawapo fit

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga SC, Miguel Gamond amesema kwenye mechi yao ya Jumatano dhidi ya TS Galaxy atahakikisha kila mchezaji anapata fursa ya kucheza huku akionesha kuridhishwa na viwango vya wachezaji wake kwenye mchezo wao dhidi ya Augsburg ya Ujerumani.

Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa Yanga kwenye kampeni yake ya pre-season msimu huu ambapo wamekita kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya wa soka 2024/25.

"Kwenye mechi hiyo nitamuweka kila mchezaji angalau dakika 45 ili kutengeneza utimamu wa wachezaji. Polepole tunatengeneza timu.

"Dube hajacheza kwa zaidi ya miezi sita, hayuko fit na anakosa vitu vingi kimchezo, hata Baleke naye hayuko fit japo ni wachezaji wazuri na wote watafaa kwa mahitaji ya Yanga, polepole wanaanza kuzoea timu na kuingia kwenye mfumo wa timu," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: